VIDEO: Baada ya kuchukua ubingwa wa NBA, Golden State Warriors wafanya yao

Baada ya kutwaa ubingwa wa NBA kwa mara ya pili mfululizo usiku wa kuamkia jana kwa kuwachabanga mahasimu wao Cleveland Cavalies kwa vikapu 108-85, Timu hiyo imefanya party ya mamilioni ya fedha.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa wachezaji hao baada ya kutawazwa ubingwa wakiwa kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo walitumia zaidi ya dola $400,000 sawa na tsh milioni 900 kwa kununua vinywaji na shampeni.
Mtandao huo umeripoti kuwa walinunua chupa 300 za MOET , hii sio mara yao ya kwanza kwani hata mwaka jana iliripotiwa kuwa walitumia dola $230,000 katika kusherehekea ubingwa wao.
Warriors inakuwa klabu ya kwanza ya NBA kwa miaka mitano kupata mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa ubingwa huo mara tatu .
Tazama video wachezaji wa Warriors wakimwaga shampeni baada ya kutwaa ubingwa wa NBA