Sakata la Shetta Kufulia 'Sijafulia Naingiza Milioni 1 Kwa Siku' Wadau Wajiuliza Anafanya Deal Gani

Staa wa muziki wa Bongo fleva Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta amefunguka na kudai kuwa hajafulia kama watu wengi wanavyodai kwani anafanya biashara inayompa kipato kikubwa tu.

Shetta alishawahi kufanya vizuri siku za nyuma na ngoma kali kama Nidanganye na Mdananda, amesema sababu tu hasikiki Kwenye muziki kwa hivi sasa haimaanishi kama amefulia.

Shetta amesema ana biashara ndogo ndogo ambazo zinamuingizia kipato kikubwa kwani hivi sasa ana vibanda vya kukaanga chipsi kama vitani ambavyo vinamuingizia kipato cha kutosha.

Mimi nafanya bishara, nina biashara ndogondogo ambazo nazikusanya pia, ujue mimi ni mmoja kati ya watu ambao wana vibanda vya chips vingi, kwa siku kila kimoja kinatoa laki na nusu au laki mbili, imagine una vibanda vya chips vitano ambavyo kila siku vinakupa laki 2, kwa hiyo nakusanaya milioni kila siku”.

Lakini pia Shetta amesema bado anaingiza pesa pia kwa njia ya muziki kwani anasimamia wasanii ambao ni The Mafik Band.