Ningekuwa Mimi ndo Daimond Ningewapiga Chini Hamisa Mobetto, Wema na Zari- Yusuph Mlela

Ningekuwa Mimi ndo Daimond Ningewapiga Chini Hamisa Mobetto, Wema na Zari- Yusuph Mlela
MSANII wa bongo Movies, Yusuph Mlela amefunguka na kusema angekuwa yeye ndo’ Diamond Platinumz, basi asingekuwa na uhusiano na Zari, Hamisa Mobeto wala Wema Sepetu lakini kwa sababu Diamond ndiyo maisha aliyoyachagua basi hana budi kuendelea nayo.

“Kiukweli mimi siwezi kumshauri kitu, Diamond ana maisha yake na maamuzi yake pia, kwa hiyo yeye afurahie tu maisha yake its ok, mimi siwezi kumpangia. Ningekuwa mimi nisingekuwa nao wote (Zari, Mobeto wala Wema), siyo kwamba siwapendi, kwanza sitembei na watu maarufu ninatoka na watu wa kawaida tu,” alisema Mlela.