Mwezi kama huu, Miaka 19 iliyopita Ja Rule alitoa Album yake ya ‘Venni Vetti Vecci’

June 1 miaka 19 iliyopita moja ya marapa wakali Ja Rule alitoa album yake ya kwanza ya Venni Vetti Vicci.

Rule alitoa album hiyo June 1, mwaka 1999 kama msanii ikiwa ni ya kwanza pia kutoka lebo ya Murder Inc. humo ndani kulikuwa na ujazo wa hali ya juu  na ilikuwa ni breathrough au kutoboa na kutoka sio tu kwa Ja Rule lakini na kwa Murder inc pia.

Ilikuwa ni moja ya album kali na inabdaki kuwa hivo na ilimpa heshima sana Ja Rule na Murder inc pia New York na duniani. sio tu heshima bali na mafanikio pia.

Album ilionesha uwezo wa Ja Rule style yake na nguvu aliyowekeza kwenye kazi na kuonesha ugumu wa East Coast na harakati zilizokuwepo miaka ya 90 na 2000.

Production ilikuwa kali na mashahiri na ugumu uliokuwepo vilifanya album kuwa ya kipekee, ingawa ilisemekana Ja hakuwa mkali sana wa kuandika! hata hivyo album hii ilifanya makabati ya kuuza nakala kuwa meupe kwa kununuliwa sana kwa kazi hiyo.


Kimauzo, album ilifanya poa sana kufanya vizuri kwenye chati kuingia mpaka nafasi ya kwanza kwenye chati mama za muziki duniani za Billboard R&B/HipHop na Billboard 200 na kufikisha Platnum katika mwaka iliyotoka. yani mauzo ya nakali million 1.

Hii ni ngoma kubwa iliyotoka kama kutambulisha album hiyo. Holla. icheki hapa. Unakumbuka nini?