Drake ameweka rekodi mpya na kuvunja ya Elvis Presley


Licha ya beef zito linaloendela kati ya Drake na Pusha T na baada ya Pusha kumpiga Diss ambayo mpaka sasa Drake hajarudisha ya The Story of Adidon na watu kuona jamaa kapigwa pigo takatifu ndani ya wiki hii lakini pia amekuwa na good news.

Drake ametangazwa na Billboard May 30 kuipita rekodi ya Elvis Presley kwenye list ya ngoma 10 bora zaidi kuwahi kutokea kwenye chati hiyo kwa upande wa wasanii wa kiume.


Hii ni baada ya ngoma ya Yes Indeed ya Lil Baby ft Drake kusogea mpaka nafasi kutoka nafasi ya 49 hadi 6 kwenye chati za Billboard Hot 100 ikiwa ni ngoma ya kwanza kwa Lil baby kuingia Top 10 kwenye chati hizo lakini imemfanya Drizzy kuwa na jumla ya Top 10 ishirini na sita (ngoma 26 zilizowahi kuingia nafasi ya kwanza zikiwa zake na alizohusika) na kuwa msanii kwenye wa 4 nyuma ya Elton John (27). Stevie Wonder (28) and Michael Jackson (29) na kumtoa Elvis Presley kwenye nafasi hiyo.

Mwaka jana tu peke yake, Drake kupitia More Life aliingiza ngoma 6 kwenye chati hizo mpaka nafasi nafasi za juu na ndani ya 10 bora, inategemewa tena Drake ataendelea kufaweka rekodi hizo kupitia album yake mpya ya Scorpion inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.