Dogo Janja "Young Dee na Young Killer Madogo Sana Kwangu Hawaoni Ndani, Niko Juu Sana'

Msanii wa kizazi kipya nchini Abdulaziz Chende maarufu Dogo Janja anayetamba  kwa kibao cha "wayu wayu" amesema bado yupo juu hashindanishwi na young D wala young Killer.

Akipiga story na Muungwana Blog baada kumaliza show kwenye uzinduzi wa UMISSETA Kitaifa mkoani Mwanza ameshukuru kwa kupokelewa vizuri na wananfunzi wanaoshiriki mashindano hayo ambapo amesema kuwa uwezo na kipaji alichonacho ndio kimeleta shangwe hizo.

"Bado mie ni mkali ndio maana na najua mashabiki wanataka nini hicho ni moja ya kitu kinachonifanya niendelee kuwa bora, amesema.

Aidha amewaomba mashabiki wa Mwanza na wadau mbalimbali wa burudani  waendelee kumsapot kwa ngoma kali anazotoa.