Baby Madaha 'Sipendi Kutoa Papa Yangu Kwa Wanaume Wakibongo ni Wababaishaji Wananitia Nuksi

Msanii wa Bongo fleva Baby Madaha amewapa makavu ya Uso wanaume wa Dar na kudai ni Matapeli wa mapenzi.

Baby Madaha amefunguka na kuwatolea uvivu wanaume wa Kibongo huku akiweka wazi kuwa kutoka na wanaume hawa ni kujitia tu nuksi kwani huishia kukupotezea muda na kukutosa.

Kwenye mahojiano na Global Publishers ,Baby  Madaha alisema kuwa watu wengi hawamuelewi kwa nini hawajawahi kumuona na mwanaume au kumnadi mpenzi wake mitandaoni kwa sababu hapendi kabisa kutoka kimapenzi na Mbongo.

Watakuja kunisikia tu nimeolewa huko nje ndio watajua ninachomaanisha, sipendi kabisa kumpa penzi Mmbongo kwa sababu wengi wababaishaji na wanajua kutiana nuksi sana kwakweli“.

Wanaume wa Kibongo nao wamekuwa wakisema hayo hayo mambo kuhusu wanawake hadi wengine hasa mastaa wa kiume wameonekana wakienda kuoa nje ya nchi kwa kuwakimbia watoto wa kike wa kibongo.