Album ya Kanye West iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa YE is finaly here. 


Kanye West ametoa album yake ya Ye ambayo kwa sasa inapatikana mtandaoni, unaweza kusikiliza kupitia Apple Music, Spotify na TIDAL.
Album hiyo imedrop kwenye mtandao siku ya Ijumaa June 1, 2018 lakini Usikilizaji wake wa album hiyo ulifanya siku ya alhamisi May 31, 2018 Jackson Hole, Wyoming kupitia WAV app.
Picha ya Cover la album hiyo imepigwa na simu (Iphone) wakati West alipokuwa njiani kuelekea kwenye listening party hiyo, ikiwa ni dakika za mwisho mwisho za kutoa album na cover ilikuwa bado! Kwa mujibu wa mke wake Kim Kardashian alisema hiyo kupitia twitter.Album hiyo ina ngoma 7 na inaurefu wa dakika 23 , angalia ngoma zilizopo.