VIDEO: Rayvanny alivyopokelewa Angola na kujibu maswali 10 aliyoulizwa kwa kireno

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny juzi May 01, 2018 alienda nchini Angola na kupokelewa na watu kibao wakiwemo waandishi wa habari na wasanii wakubwa nchini humo.
Rayvanny alipofika uwanja wa ndege wa kimataifa nchini humo wa Quatro de Fevereiro, alidakwa na waandishi wa habari ambao walifanya naye mahojiano kwa lugha ya kireno.
Mahojiano hayo yaliyodumu kwa dakika 12, yaliendeshwa kwa lugha ya kireno na kutafsiriwa kwa kiingereza kabla ya Rayvanny kujibu na baadaye Rayvanny akaondoka na wenyeji waliokuja kumpokea uwanjani hapo.
Rayvanny yupo nchini Angola ku-shoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii mkubwa wa kike nchini humo, N’soki.
Tazama mapokezi yake hapa chini na mahojiano yake (Video by Jnz News Tv)