Utani wa Barnaba kwa Billnass “Nakuogopa Labda Uje Mikono Umekata”

Utani wa Barnaba kwa Billnass “Nakuogopa Labda Uje Mikono Umekata”

Leo May 3,2018 kutana na comment ya staa wa muziki wa Bongo Fleva Barnaba akimjibu Billnas kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amepost video ya msichana ambaye inasemekana ndiye mpenzi wake wa sasa wakiwa pamoja studio .

Billnass baada ya kuona post hiyo aliamua kuandikia comment inayosema >>>“Kaka upo nae studio hapo? nataka nije kurecord kaka ile ngoma yetu classic ndio muda wake” na baada ya muda Barnaba alionekana kumjibu Billnass na kusema “studio nimefunga mdogo wangu kwa muda nakuogopa sana mdogo wangu labda uje mikono umekata”

Kutokana na comment hiyo ya Barnaba mashabiki wengi wameihusisha na video ya Billnass na Nandy iliyovuja na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha wakiwa mapenzini siku kadhaa zilizopita.