Tyson Kurudi Tena Ulingoni Mwezi Ujao

Tyson Kurudi Tena Ulingoni Mwezi Ujao
Bingwa wazamani wa uzito wa juu Duniani, Tyson Fury anatarajia kurejea tena ulingoni Juni 9 kumkabili bondia, Albanian Sefer Seferi dimba la Manchester Arena.

Fury ambaye ni bingwa wa IBF, WBA na WBO ataingia ulingoni baada ya kukosekana kwamuda wa miaka miwili na nusu kufuatia kukutwa na tuhuma za kutumia madawa yaliyokatazwa michezo.

Bondia huyo wa Uigereza mwenye mapambano 25, akishinda yote na 18 ikiwa ni kwa njia ya KO atamkabili, Sefer Seferi mwenye umri wa miaka 39.

Mara ya mwisho Fury aliingia ulingoni Novemba mwaka 2015 alipomkabili bondia, Wladimir Klitschko wakati, Seferi akipoteza mbele ya Manuel Charr Septemba mwaka 2016.