Thea afunguka hakuna staa mpya anayempa changamoto


MKONGWE kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ ambaye kwenye gemu amedumu kwa miaka 20 sasa amedai kuwa hakuna staa yeyote wa sasa anayempa changamoto kiasi cha kumtisha.

Akiongea na safu hii Thea ameeleza mengi lakini pia akaweka wazi jinsi anavyoweza kuulinda ustaa wake akidai ni kwa kutengeneza kazi nzuri ambazo zinahitajika sokoni.

MSIKIE MWENYEWE 
“Nina miaka 20 kwenye gemu hili, sina changamoto yoyote ninayokumbana nayo kwa mastaa wa sasa lakini naweza kuwaambia wafanye kazi kwa bidii kwani gemu hili kudumu kwa miaka hiyo ukiwa bado unafanya kazi nzuri na zinalipa ni gumu sana.”

ANA FILAMU NGAPI MPAKA SASA?
“Nina filamu zaidi ya hamsini mpaka sasa, miongoni mwa hizo ni Ukungu, Dadaz, Malaika, Jiwe, Kipusa, Sengoto, Moses, Revanger, Bad Rest, Good Fellow, Sikitiko Langu, Born to Suffer, Selura na Suspenser.” Katika zote hizo mwenyewe anaeleza kuwa anaipenda sana Sengito.

ANAVYOPENDELEA
Alisema amekuwa akijipenda lakini analala saa sita kama hana kazi, akiwa na kazi za kuandaa filamu hulala saa tisa.

Chakula anachokipenda ni pilau, mandazi na kuku, lakini pia ndio anapenda kupika chakula hicho miongoni mwa vyakula vyote.

USHAURI KWA MASTAA
Wafanye kazi kwa kujituma sana, waachane na skendo