Romy Jons Kuachia Albamu Yake Ambayo Amewashirikisha Wasanii wa Afrika na Marekani

Romy Jons Kuachia Albamu Yake Ambayo Amewashirikisha Wasanii wa Afrika na Marekani
Romy Jons ambaye ni Dj wa Diamond Platnumz, amefunguka kuhusu albamu yake ambayo amepanga kuiachia mwaka huu.

Akiongea na Kiss FM, Romy ambaye tayari ameshaachia wimbo mmoja aliomshirikisha Barakah ambao unatajwa kuwa kwenye albamu hiyo, amesema albamu hiyo inaladha ya staili tofauti ikiwemo Hip Hop, RnB, Ragger.

Pia ameongeza kuwa kwenye albamu hiyo amewashirikisha wasanii kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria na Marekani. “Albamu yangu nadhani mwezi wa sabab nitasema rasmi inatoka lini, albamu yangu ipo tayari na kila siku zinavyozidi kwenda naipeleka mbele. Kizuri katika albamu yangu hakuna Bongo Fleva peke yake, kuna Bongo Fleva, Hip Hop, RnB, Ragger, yaani kun itu vingi vya tofauti kwa sababu kuna wasanii wengi watofauti,” amesema Romy.

“Kunawasanii wengi watofauti kutoka Dar es Salam, Kenya, Uganda, Nigeria na Marekani,” ameongeza.