Rayvanny na Khaligraph Jones kwa mara nyingine tena

Rapper kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones ni miongoni mwa wasanii wataokao kuwepo katika remix ya ngoma ya Rayvanny ‘Pochi Nene’
Hadi sasa wasanii ambao Rayvanny ameweka wazi kuwepo katika remix ya ngoma hiyo ni pamoja na Bill Nass na Country Boy. Original version ya Pochi Nene amefanya Rayvanny na producer S2kizzy.
Utakumbuka Rayvanny na Khaligraph Jones walishatoa ngoma ya pamoja inayokwenda kwa jina la Chalii ya Ghetto. Hadi kufikia sasa Khaligraph amefanya kolabo na wasanii wa Bongo kama Nikki Mbishi, Christian Bella, Chin Bees, Rosa Ree na Young Killer.