Q Chief Amtupia Lawana B Dozen "Nilishawahi Kumfuata Anisaidie Lakini Haikuwezekana"


Katika maelezo yake #QChief anasema kati ya watu ambao aliwatafuta sana ili kupata msaada wakati muziki wake unaenda vibaya ni Mtangazaji @bdozen. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali Chilla anasema hakupata msaada aliotarajia kutoka kwa Dozen.

Katika kueleza hilo Dozen alisema. "Katika kipindi ulichonifuata nikusimamie sikuwa naweza kufanya hivyo. Ilifika kipindi wewe pia uliacha kunisukuma na unajua kuna majukumu mengi nafanya. Lakini hapa tuongee kitu cha maana ili kuendelea mbele..... Mimi kama Dozen nakupa ahadi kama leo utasitisha uamuzi wako wa kuacha muziki, nakupa ahadi ya kukupa mchango wa mawazo, mbinu na kadri nitakavyojaaliwa ili kukusaidia kurudi unapostahili. Lakini siwezi kukuahidi kwamba tutatengeneza hits.” @bdozen.