Picha: Show ya Diamond ilivyotikisa mjini London

Usiku wa jana Diamond aliwasha moto kwenye show yake iliyofanyika katika ukumbi wa The Royal Agency uliopo mjini London nchini Uingereza.

Kwenye show hiyo hit maker huyo wa African Beauty, alifanikiwa kujaza nyomi ya watu kwenye ukumbi huo ambao wengi wao walionekana kuwa ni wenye asili ya Afrika.
 
Usiku wa leo hit maker huyo wa African Beauty, anatarajia kutumbuiza Birmingham katika ukumbi wa Sport Complex. Diamond kwa sasa anamfululizo wa show takribani 22 ambapo ya mwisho itakuwa ni One Africa Dubai itakayofanyika Novemba 16 ya mwaka huu.