Nikiwa Tajiri Nitaongeza Watoto Wengine 10- Faiza Ally

Nikiwa Tajiri Nitaongeza Watoto Wengine 10- Faiza Ally
Msanii Faiza Ally ambaye pia ni mama wa watoto wawili amesema kuwa ataongeza watoto wengine endapo akiwa tajiri.


Faiza amesema hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv ambapo amesema kuwa kwa sasa hali yakekiuchumi inamtosha kuwa na watoto wawili tu na endapo akitajirika atafikisha hata kumi ikiwezekana.

“Kwa uwezo wangu kwa sasa ni wawili tu lakini mwenyezi Mungu akinijaalia kipato zaidi ya hiki nitazaa hata kumi kwa sababu na penda watoto sana”. Amesema Faiza

Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 34 amejizolea umaarufu kupitia baadhi ya matukio anayofanya mitandaoni hali iliyopelekea simu yake ya mkononi kushikiliwa na jeshi la Polisi kutokana na kupost picha ikimuonesha wakati akijifungua mtoto wake wa pili.