Nicki Minaj Atoa Video Mbili Kwa Mpigo

STAA wa kike wa Muziki wa Hip Hop, Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’ Baada ya kupita miezi minne bila ya kuachia ngoma mpya, mekuja kwa hasira kwa kuachia video mbili kwa mpigo.
Rapper huyo ameachia video ya wimbo wake ‘Chun-Li’ na ‘Barbie Tingz’. Wimbo wake wa mwisho ulikuwa ni Motorsport ambao aliimba na Migos pamoja na Cardi B. Mpaka sasa video ya Chun-Li imeshatazamwa zaidi ya milioni tano kwenye mtandao wa YouTube, wakati ‘Barbie Tingz’ ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni tatu. Tazama hapa chini video zote mbili