Mtoto wa Kylie Jenner Atakiwa Kupimwa DNA

Mtoto wa Kylie Jenner atakiwa kupimwa DNA
Bi. Wanda Webster ambaye ni mama mzazi wa msanii Travis Scott aliyezaa na Kylie Jenner, ametaka mtoto aliyezaliwa na wawili hao kupimwa vinasaba, ili kuthibitisha kama mtoto wake Travis ndiye baba mzazi.


Mama huyo amefikia uamuzi huo mzito baaada ya Kylie kupost picha ya mtoto wake na Travis anayeitwa 'Stormy', na watu kusema mtoto huyo amefanana na mlinzi wa Kylie Tim Chung.

Bi. Wanda anaamini kwamba mtoto wake Travis sio baba mzazi wa Stormy, baada ya watu kuibua maneno mitandaoni kwamba mtoto huyo hajafanana hata kidogo na rapper huyo, na badala yake amefanana na mlinzi wa Kylie Jenner ambaye muda mwingi huwa naye.

Licha ya uamuzi wa mama yake Travis kutaka kufanyika DNA kwa mjukuu wake, wazazi wa Stormy ambao ni Travis na Kylie wameonesha kudharau maneno ya watu wakisema hayana ukweli wowote.