Mrembo Kikojozi Bongo Movies Afunguka..Adai Watu Wanamzushia

Muigizaji wa filamu Bongo Mwanaheri Afcely kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya tuhuma za kuwa kikojozi.


Akizungumza na www.eatv.tv, Mwanaheri amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote na watu walioanzisha hizo habari wana wivu juu ya ndoa yake.

“Hakuna ukweli wowote, sijawahi kujikojolea hata siku moja, mimi ni msanii huwa nalala kambini, wapigie simu kina JB waulize kama kuna siku nimewahi kukojoa, jamani hii ndoa watu imewauma, mpaka kunizushia habari za uongo!! Sio kweli mimi sio kikojozi, ila nina tatizo la pumu tangu utotoni”, amesema Mwanaheri.

Eatv ilizinyaka taarifa za mlimbwende huyo aliyejaliwa shepu ya kiafrika kutoka kwa mmoja wa watu wake wa karibu, na kusema kwamba msichana huyo ana tatizo la kujikojolea kitandani alilokuwa nalo tangu utotoni.