Michepuko kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida – Young Killer

Rapper Young Killer mara baada ya kusikia aliyekuwa mpenzi wake ‘Halimaty’ kwa sasa ana ujauzito wa mtu mwingine, amevunja ukimya.

Young Killer akipiga stori na U-Heard, Clouds FM amesema jambo hilo halimuumizi kwani walishaachana na siku zote kila chenye mwanzo kina mwisho wake.
 
Pia Young Killer amekanusha taarifa kuwa kipindi cha mahusiano yao alikuwa akimnyanyasa mrembo huyo.
 
“Hapana, ni maneno ya watu hayo kwa sababu matatizo madogo madogo, sijui michepuko huwa ni vitu vya kawaida kwenye mapenzi, huwa havikosi, umenisoma?,” amesema Young Killer.
 
“Ni jambo la kheri, hapana siumii kwa sababu hakuna kitu kama kuona mtu ambaye mlikuwa mnapeana furaha anaendelea kufurahi,” ameongeza.
Kipindi cha mapenzi yao kabla ya kuchana
Young Killer ambaye anafanya muziki wake chini ya Wanene Entertainment kwa sasa anatamba na ngoma ‘Shots’ aliyomshirikisha rapper Khaligraph Jones kutokea nchini Kenya.