Mamilioni Yatakayotumika Kwenye Birthday Party Ya Mtoto Wa Chris Brown

Chris Brown ametajwa kwenye vichwa vya habari baada ya taarifa iliyohusisha Birthday Party ya mtoto wake Royalty kutolewa.

Kinachomuingiza tena Breezy kwenye headlines ni mkwanja mrefu unaotarajiwa kukamilisha sherehe hiyo siku ya jumapili, Mei 27.

Dola 30,000 za Marekani (sawa na 6.7M Za Kibongo) zimetajwa kama pesa zitakazokamilisha party hiyo.

Kwa mujibu Wa TMZ Breezy ameweka tofauti zake pembeni na Mama mzazi Wa mtoto wake (Nia Guznam) ili kujumuika naye pamoja kwenye birthday Party ya mtoto wake.

Nia na Breezy wamefikishana mahakamani mara kadhaa huku chanzo kikiwa ni umiliki halali wa mtoto wao ambaye amekuwa akilelewa na Chris Brown tangu kuzaliwa kwake mwaka 2014.

Disney's Princesses ni miongoni mwa wageni waalikwa wengi watakaohudhuria sherehe hiyo.