Mama wa Jay-Z: Nilimwambia Mwanangu Nina Mpenzi wa Jinsia Moja

Mama wa Jay-Z: Nilimwambia Mwanangu Nina Mpenzi wa Jinsia Moja
Mama yake mwanamuziki maarufu nchini Marekani na duniani, Jay- Z amezungumza namna ambavyo mtoto wake amekuwa akimpa moyo alipomwambia kuwa amekuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Gloria Carter aliiambia hadhira katika tuzo za GLAAD kuwa ni mara ya kwanza kuzungumza na mtu kuhusu ukweli wake

Mama wa watoto wanne alitunukiwa tuzo akitambuliwa kwa mchango wake kwenye wimbo uitwao Smile uliotolewa mwaka jana.

Alisema: ''Smile imekuwa halisia kwa sababu nilimshirikisha mtoto wangu nikimweleza mimi ni nani.''

''Mtoto wangu alilia na akasema: 'lazima maisha yalikuwa mabaya sana kuishi namna hiyo kwa muda mrefu.''

''Maisha yangu hayakuwa mabaya,''aliongeza.

''Nilichagua kuilinda familia yangu.Nilikuwa na furaha japo sikuwa huru