Jinsi Heineken ilivyonogesha Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions League jijini Dar


  • Fursa hii ya aina yake iliwalenga wapenzi wa soka, wateja wa Heineken Tanzania na ilifanyika katika sehemu nane  tofauti nchini
  • Heineken imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na itaendelea kuwa mmoja wa wadhamini wakubwa wa ligi hiyo  hadi kufikia mwaka 2021
Dar es Salaam, Mei 28 2018: Ulikuwa ni usiku wenye shamra shamra na msisimko wa aina yake pale ambapo wapenzi wa soka, na watu maarufu walipokutana kwa pamoja Msasani jijini Dar es Salaam kushuhudia fainali za Klabu Bingwa  Barani Ulaya kwa mwaka 2018.
Zaidi ya mashabiki 2600 wa Kitanzania, waliweza kufurahia fursa ya kipekee ya kutazama fainali hizo katika mazingira safi ambapo miamba wa soka Liverpool kutoka nchini Uingereza walikutana na miamba wa Hispania Real Madrid. Katika mtanange huo Real Madrid .walitawazwa mabingwa baada ya kuwalaza Liverpool .kwa mabao 3 – 1.Ikiwa mmoja wa wadhamini wakuu wa ligi hiyo maarufu na inayotizamwa na mamilioni ya watu kote duniani, Heineken iliweza kuwaleta pamoja Watanzania chini ya bia yao pendwa ya Heineken na kupata fursa ya kutazama fainali hizo.

Meneja wa Heineken Afrika  Mashariki Njeri Mburu alisema,  “Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni moja kati ya ligi zinazohusisha wachezaji wakubwa. Timu zote bora barani Ulaya zinashiriki ligi hii. Kwa uapnde mwingine, bia ya Heineken ni bia inayojulikana na kutumiwa na watu wengi kote duniani  na kwa hiyo kuna uhusiano kati ya Heineken na ligi ya mabingwa. Mwaka huu, wateja wetu siyo tu hawatafurahia kutazama ligi bali pia kushiriki fursa zinazokuja na ligi,”

Aliongeza  “Bia ya Heineken inatengeneza msisimko katika ligi hii kubwa duniani kwa kuwaleta pamoja kwa mamna ya pekee ambayo ni Heineken tu wanafanya. Kwa Tanzania, Heineken imetoa haki za kipekee kwa mashabiki kuweza kushirikia katika kutizama fainali katika mazingira tulivu na ya aina yake kwenye maeneo mbali mbali kama Red Sea Arena, George &  Dragon na Club 777.  Fainali hii pia ilitizamwa katika shehemu tofauti tofauti  8 katika shehemu mbali mbali nchini,”
Njeri aliongeza kuwa, wateja wa Heineken waliweza kushiriki pamoja na kubadilishana taarifa za matukio wakati wakitazama fainali kupitia kibwagizo  #ShareTheDrama
“Tunafurahi kuwa bia ya Heineken ni bia ya Watanzania na siku zote wamekuwa sehemu ya kile tunachokifanya na hata wanam kunywa zaidi bia yetu,” aliongeza
Alisema ikiwa kama bia yenye jina kubwa, siku zote imekuwa ikidhamini na kuwekeza kwenye michezo ambayo inayowagusa wateja wake na kuwaleta pamoja katika masoko yanayochipukia kama Tanzania.
Wakati wa fainali hizo, Heineken iliwazawadia wateja wake bidhaa mbali mbali zi zinazotokana na ligi hiyo. Taarifa zinapatikana kwenye www.facebook.com/Heineken na Twitter https://twitter.com/Heineken_TZ
TAARIFA KWA WAHARIRI
  • HEINEKEN I imekuwa mdau wa UEFA tangu mwaka1994
  • Mwaka 2005, Heineken iliichukua HEINEKEN iliyokuwa inamilikiwa na Amstel
  • Heineken italeta udhamini kwa nchi zaidi ya 220 kupitia kampeni za kimasoko na mawasiliano kwa umma.
  • Ligi ya Mabingwa inatazamwa na zaidi ya watu bilioni 4.2 kote duniani.
  • Tangu mwaka 2007, kombe la UEFA linalotembezwa na Heineken, limefika zaidi ya nchi 35 ikiwamo Afrika, Asia Amerika ya Kaskazini na Kusini
  • Kufuatia kusainiwa kwa mkataba mpya, Heineken itaendea kuidhamini UEFA hadi kufikia msimu wa mwaka 2020/2021.