Janet Jackson Aweka Histolia Apata Tuzo ya Heshima ya Billboard Awards

Janet Jackson Aweka Histolia Apata Tuzo ya Heshima ya Billboard Awards
Staa mkongwe katika game ya muziki nchini Marekani Janet Jackson ameingia katika historia nyingine baada ya kuwa mwanamke Mmarekani mweusi kupata tuzo ya heshima kwenye tuzo za Billboard Awards zilizofanyika usiku wa Jumapili May 20,2018, Marekani.

Katika historia hiyo Janet Jackson anakuwa mwanamke wa nne kupata heshima hiyo tokea tuzo hizo kuanzishwa mwaka 2011 ikiwa mastaa watatu waliwahi kushinda tuzo hiyo akiwemo Celine Dion, Jennifer Lopez na Cher maarufu kama “The Goddess of Pop”

Janet Jackson mwenye umri wa miaka 52 alianza kazi yake ya muziki mwaka 1973  na ametambulika zaidi kutokana na kuwa dada wa Marehemu Michael Jackson(King Of Pop) na pia kutokea kwenye familia ya Jackson 5.