Foleni ya wanaume wanaotaka kuwa na mimi hutoiamini – Zari

Zari The Boss Lady amesema licha ya idadi kubwa ya wanaume kuhitaji kuwa katika mahusiano na yeye bado hayupo tayari.
Mrembo huyo ambaye anaaminika kuwa na mkwanja mrefu zaidi amesema kwa sasa mambo yote ni yeye na watoto wake tu. Kupitia mtandao wa Snapchart ameandika;
Oooh anajinunilisha magari kwa sababu hana raha, hapana sio kweli dada, nipo single kwa sababu nimeamua kuwa hivyo kwa sasa, foleni ya wanaume wanaotaka kuwa na mimi hutoiamini lakini ninafurahia maisha kwa sasa nikiwa tayari nitaweka wazi lakini kwa sasa ni mimi na watoto wangu tu.

Kauli hiyo ya Zari imekuja mara baada ya kununua gari aina ya Range Rover Spor na kuibuka stori kuwa huenda mrembo huyo kapata mwanaume ambaye ameamua kumuhudumia vilivyo.
Utakunbuka mnano February 14 mwaka huu katika siku ya wapenda nao Zari The Boss Lady ambaye ni mzazi mwenzie na Diamond Platnumz, aliposti Ua Jeusi katika mtandao wa Instagram na kutangaza kuachana kimahusiano na msanii huyo rasmi.