Fahamu vigezo Anavyovipenda Chemical kwa Mwanaume

Rapa wa kike nchini Claudia Lubalo maarufu kama ‘Chemical’ amefunguka kuwa anapendezwa zaidi na mwanaume mrefu na asiye na kitambi.

Chemical amesema hayo kupitia KIKAANGONI ya EATV kuwa mwanaume mwenye vigezo hivyo wanamvutia zaidi kuliko wafupi na wenye miili mikubwa.

“mwanaume akiwa mfupi hatoweza kuni-kiss na wala asiwe mnene wala mwembamba awe kawaida tu na wala asiwe mbeba vyuma”, amesema Chemical

Aidha Chemical ameongeza kuwa anapenda mwanaume ambaye atamkubali yeye kama yeye na si kutaka abadili muonekano