Davido kaonyesha ukweli juu ya gari aliyomnunulia mpenzi wake

Mara baada ya Mwanamuziki Davido kumnunulia gari kifahari aina ya Porshe mpenzi wake Chioma,kwenye siku ya kuzaliwa kwake,ku mekuwa na maneno maneo kuhusu Nyaraka za gari hiyo je zina jina la nani kwani gari hiyo ni gharama kubwa.


Mwanamuziki huyo mara baada ya kusikia maneno mengi yaliokuwa yakitawala kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria ,Mwanamuziki huyo jana alithibitisha kuwa gari hiyo amemnunulia mpenzi wake chioma na majina ya nyaraka za gari hilo ni ya Chioma .

 
Mwanamuziki huyo aliweka hayo bayana na kuonyesha nyaraka hizo alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari Jijini Lagos Nigeria.pia alithibitisha hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter