Chris Brown amchana Kanye West kupitia mahojiano ya Will.i.am

Msanii wa muziki nchini Marekani, Chris Brown ameamua kumtolea uvivu rapa Kanye West kwa kumwambia kuwa abadilishe mwenendo wa maisha yake awe kama kiongozi.


Chris Brown ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa kuposti video ya rapa wa kundi la Black Eyed Peas, Will.i.am ikimuonesha akimkosoa Kanye West kwa kauli yake ya “Watu weusi kutawaliwa miaka 400 walipenda” aliyoitoa juzi Mei 01, 2018 kwenye mahojiano yake na TMZ .

Chris Brown amempongeza Will.i.am kwa kumwambia kuwa alikuwa anawaza namna ya kufikisha ujumbe lakini kwa interview yake (Will.i.am) imeongelea kila kitu ambacho alitaka kuongelea juu ya kauli ya Kanye West.

Amefunguka sana kuliko hata mimi pengine ambavyo nimefanya kwenye post yangu ya kwanza ambayo nimeifuta kwa sababu imepokelewa ndivyo sivyo, nataka Kanye uwe kama kiongozi na sio kama Kigong’ota.“ameandika Chris Brown kwa kumfananisha Kanye na aina ya ndege.
Tokeo la picha la chris brown and kanye west