Boyfriend wa Cardi B, Offset wa MIGOS apata ajali, Alazwa Hosipitali

Member wa kundi la Migos, Offset na mchumba wa Cardi B amepata ajili ya gari na kulazwa hospitali.Rapa huyo wa kundi hilo la Migos aligonga gari yake ya kijani aina ya Dodge Challenger siku ya Jumatano (May 16) Atlanta, na kuwahishwa hosptali. source za TMZ zinasema alipata majeraha madogo na anaendelea vizuri.


Anategemewa kupona na kuwa sawa lakini gari yake imeharibika vibaya sana.


Hakuna polisi wala matibabu ya dharula na wala hakuna ripoti ya traffic ya ajali hiyo iliyochukuliwa!!! 

Baada ya jali hiyo kutokea, mchumba wake Cardi B aliwahi fasta kuwa karibu na mchumba wake huyo na baadae kuandika kwenye twitter “@OffsetYRN i love him Soo much,” aliandikiwa na kuweka emoji za maombi.

Cardi na Offset wanategemea kupata mtoto mwezi wa saba kwani tayari anaujauzito wa miezi saba.