Babu Tale Aendelea Kusota Mahabusu...Kesi yake Bado Nzito


Mkurugenzi wa Kampuni ya Tiptop Connection Limited, Hamis Shaaban Taletale maarufu kwa jina la Babu Tale na mwenzake Iddi Tale wameendelea kukaa mahabusu katika kituo cha Polisi wakisubiri amri ya kupelekwa kifungoni

Babu Tale na ndugu yake Idd Taletale waliamriwa kumlipa fidia ya Shilingi Milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kwa makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake

Kutokana na kushindwa kulipa kiasi hicho cha pesa, Sheikh Mbonde aliwasilisha maombi ya kuwafunga jela ambapo mahakama imemwelekeza kuwalipia wafungwa hao watarajiwa fedha za chakula na matumizi mengine

Sheikh Mbonde tayari ameshawalipia wafungwa hao fedha za chakula za mwezi mmoja kiasi cha takribani Shilingi Milioni 1 sambamba na shilingi milioni 1 na laki 6 za dharula na kusema ataendelea kuwalipia kiasi kama hicho kila mwezi - #regrann