AUDIO : Quentin Miller Kamjibu DRAKE kwenye 'Destiny' Freestyle I Beef Pusha T na Drake


Beef zito zinaloendelea katika game ya Hip Hop Marekani ni Drake na Pusha T, baada ya Pusha T kumchana Drake kwenye infrared na kusema Drake hawezi kuadnika ngoma, anatumia waandishi (Ghostwriters) kumpigia wino.

Tuhuma kama hizo aliwahi kuzileta Meek Mill kipindi cha nyuma na lilikuwa beef zito sana mpaka Drake zikawa haziivi kabisa na Nick Minaj ambaye walikuwa wana sana (Young Money)

Sasa Baada ya Pusha kumchana Drake, haikuchukua muda Drake akajibu kwenye freestyle yake ya Duppy Freestyle kama kawaida yake alichofanya kipindi cha nyuma kwa Meek Mill kwenye Headline freestyle. 

Kipindi Drake ametoa Duppy freestyle na kuwa gumzo mtandaoni na watu wengi hadi wana Hip Hop kuona Drake amefanya unyama sana, Pusha T hakurudisha majibu (yani hakutoa ngoma yoyote kujibu, kama akawa kasanda hivi.

Nick Minaj aliingilia ishu hii safari hii na kusema nyie mnaotaka kuleta ishu za Quentin eti Drake hawezi kuandika au kuwaandikia wasanii wengine, mnachokoza mzimu, unaamsha dude. mtaendelea kufanya remix na kurudia ngoma za zamani.

Kama vile Nick anamchana Pusha T na Quentin Miller na ni kama vile pia Nick anamchana Ex-Boyfriend wake (Meek Mill)

Muda kidogo baada ya Tweet ya Nick Minaj, Drake akatoa ngoma nyingine I'M UPSET, wakati huo Pusha hajarudisha na kuonekana kama Drake ameshinda hivi kwenye uwezo wa kutoa battle songs.

Sasa jamaa ambaye anadaiwa kuwahi kumuandikiwa Drake, Quentin Miller alisema kuwa ataweka wazi kila kitu na ushahidi kuwa Drake anaandikiwa ngoma, Addressing everything with this next one.... Once and for all... Quentin alisema kupitia Twitter.


Baada ya jina lake kutajwa kwenye Tweet ya Nick Minaj, jamaa huyo Quentin Miller ameingilia beef la Pusha T na Drake na kumchana Drake baada ya kuandika kwenye Twitter kuwa ataweka wazi ishu zote za Drizzy kuandikiwa ngoma.

Quentin Miller ametoa freestyle yake, Diss kwa Drake inaitwa Destiny (Hatima) isikilize hapa. Kwa story kuhusu beef hili, angalia story za Pusha na Drake zilizopita hapa.