Amber Rose Amtibua Nicki Minaj

Amber Rose
MWANAMITINDO na muuza nyago kwenye video za muziki, Amber Rose amemtibua staa wa kike wa Muziki wa Hip Hop, Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’ baada ya kuposti picha akiwa na wigi feki.
 
Kupitia Mtandao wa Snapchat, Amber aliposti picha akiwa amevalia wigi feki huku akiwa amefanana na Nicki kwa kiasi kikubwa kisha akaandika ‘caption’ yenye tusi la kujichukia.
Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’
Hata hivyo, taarifa za kuposti picha hiyo zilimfikia bidada Nicki ambapo aliandika kwa hasira kwenye Snapchat yake.
“Amber acha kunifuatilia. Nitakuona kwenye Coachella. Huwezi kuwa na nguvu kama hizi.” Kisha akaatachi na picha.
 
Inaelezwa kuwa chanzo cha bifu kilianza mwaka 2010 ambapo Nicki alimuimba Amber katika wimbo wake wa Monster.