Amber Lulu Apata Dili la Kutangaza Bidhaa za Kondomu.

Amber Lulu Apata Dili la Kutangaza Bidhaa za Kondomu.
Msanii wa muziki Bongo na video vixen, Amber Lulu amepata dili la kutangaza bidhaa za kondomu.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Jini Kisirani’ alisaini dili hilo hapo jana na kueleza kuwa linampatia fedha za kutosha.

“Nimepata mpunga mrefu nimshukuru Mungu, ni hatua moja ambayo nimepiga, so inabidi tushukuru Mungu wote,” amesema Amber Lulu.

Utakumbuka siku za nyuma kulikuwa na taarifa za ujio wa bidhaa za kondomu kutoka kwa rapper Joh Makini hata hivyo kumekuwa na ukimya wingi wa hilo.