Amber Lulu Ametaja List ya Mastaa wote Bongo Aliowahi Kutoka nao

Muimbaji wa Bongofleva Amber Lulu leo kupitia mahojiano yake na kipindi cha Break cha Clouds TV amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kukubali kuweka wazi orodha ya mastaa wa Bongo ambaye amewahi kutoka nao kimapenzi.
Amber Lulu akihojiwa na Simple The Boy aliulizwa vipi anatoka kimapenzi na Nuh Mziwanda na alikanusha  lakini alipoulizwa  ni mastaa gani wa bongo ambao amewahi kuingia nao katika mahusiano ya kimapenzi alikuwa radhi kusema.
“Mimi na Nuh  ni marafiki tu na tumefanya kazi pamoja list ya mastaa ambao nimewahi kulala nao ni Barnaba, Aslay, Rammy Garis ila Young Dee sio sana lakini Prezoo ni mume wangu unajua nampenda tu naomba anisamehe tu” Amber Lulu