Zaiid akana kuachia ngoma mpya


Rapa aliyesumbua airwaves kwa ngoma yake maarufu “Wowowo”, ZaiiD amesema hajaachia wimbo wowote mpya mpaka sasa kama ambavyo inaripotiwa na platforms tofauti kuwa ana ngoma mpya.

Amethibitisha kwenye mahojiano na Dream Fm - Mbeya kuwa “Kwenye Mdundo” Sio ngoma mpya bali ni wimbo ambao unapatikana kwenye kanda mseto (mixtape) yake ya kwanza iliyomtambulisha kwenye music Industry.

“Sijui nani ameamua kufanya hivyo kwani hiyo ni track ya miongoni mwa zile 13 za mwaka 2013 na nilitumia sana midundo ya nje ya bongo, ujio wangu soon kwenye redio na runinga”. alisema ZaiiD.

Pia amesema kuwa, kuwa busy na shows kipitia wimbo wake “Wowowo” ndio sababu ya kuchelewa kurudi na pini jipya ila kwasasa anasitisha kazi zote ili adhihirishe kuwa hakuhatisha.