Wizkid atoa sababu za kutopost picha za Drake

Baada ya WizKid kufanya collabo na Drake, wapenzi wa muziki waliishia kumtupia maneno juu ya kwanini haku-share picha zake na Drake ambaye ni msanii wa kimataifa. Sio picha tu, Staa huyo wa muziki nchini Nigeria, alishambuliwa tena baada ya Drake kukosekana kwenye video yake, Come Closer.

Wizkid ameibuka na kujibu tuhuma zote kupitia Interview na Hip TV.
"Unajua idadi ya watu ninao - hang out nao kwenye mizunguko yangu ya kila siku na si-post picha zao? Unajua idadi ya watu ambao ni marafiki zangu wakubwa tunaongea na watu hawajui kuwa ni rafiki zangu? Wako wengi tu, lakini si-post picha zao, Sijali sana kuhusu picha, Mimi naweka mawazo yangu kwenye kazi. Muziki ndio kila kitu." Alisema wizkid