Wema Sepetu afarijiwa, ‘kuitwa mama sio lazima uzae’

Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameelezwa kitendo cha kutopata mtoto hadi sasa kisimkatishe tamaa kwani wakati wake utafika Mungu akipenda.

Hayo yamesemwa na Mjasiriamali, Maznat Bridal ambapo amemueleza Wema kuwa kuitwa mama sio lazima awe na mtoto. Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;

“Kuitwa mama siyo lazima uzae, ukifikia umri tu wa kuitwa aunt, mama mdogo, shangazi, mama mkubwa ina maana wewe tayari ni mama. Kuwa mama siyo lazima uingie labour, mimi namshukuru Mungu nimezaa na nimelea watoto wangu na wasio wangu na katika yote nimejifunza kupenda watoto kwa dhati pasipo kubagua,” amesema.

“Mungu ni msiri sana sana mdogo wangu Wema Sepetu anajua nini kinamstahili nani, kwa muda gani, muda wa Mungu ukifika ataku suprise, atakupa faraja ya ajabu, atakupa kile moyo wako unahitaji, atakutunuku zawadi ya kipekee…utabaki mdomo wazi, ukishangaa maajabu ya Muumba. Jipe moyo, it is well,” amesisitiza.

September mwaka jana Wema Sepetu alieleza kuwa amekuwa akihitaji mtoto toka akiwa na umri wa miaka 24 hadi sasa ila hilo haliwezi kumkatisha tamaa. February 2016 wakati Wema akiwa katika mahusiano na muigizaji Idris aliweka wazi kubeba ujauzito wa watoto mapacha hata hivyo baadaye ujauzito huo uliripotiwa kuharibika.