Video:Diamond, Nandy Waomba Radhi Kwa Yote Yaliotokea, TCRA

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema kuwa kwa yale yote yaliomtokea ya kuachia video zilizokosa maadili kwenye mitandao ya kijamii amejifunza mengi na kwamba kilichotokea alikuwa hajui sheria za mitandao hivyo alikuwa akijipostia tu kumbe alichokuwa akiposti mashabiki walikuwa wakichukua na kuweka kwao kwa hiyo yaliotokea avumiliwe.

Diamond aliyazungumza hayo leo Alhamisi alipoitwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) pamoja na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ ambao wiki iliyopita video zao zilizokosa maadili zilisambaa mitandaoni.