VIDEO: Zari amuita Diamond ‘mjinga’

Kwenye video ya uchambuzi aliyofanya SKY anaonekana kuwa Zari ana dukuduku zito na Diamond baada ya wawili hao kuachana siku ya Valentines mwaka huu kwa Zari kuatangaza kupitia instagram na kuposti ua jeusi na kuandika ujumbe wa kuachana na Diamond.

Mapema leo kupitia Snapchat ya Zari imeonekana amerusha dongo kwa meneja wake na Diamond na wengi wakihisi ni Sallam na kuonekana kumwita Diamond mjinga! Kipindi chote toka February 14, Diamond hajasema chochote kwenye instagram yake kuhusu kuachana na Zari lakini aliweza kulitolea ufafanuzi kidogo swala hilo kwenye interview aliyofanya kwenye The Playlist, Times FM na kutangaza ndoa mwaka huu.