MWANAHERI AMEOLEWA NA BABU? MAJIBU YAKO HAPA!

Kutokana na watu mbalimbali kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii wakisema kwamba ameolewa na mwanaume mkubwa zaidi ya baba yake mzazi ‘babu’, staa wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ amewafunga midomo wanaomsema kwa kuwaeleza kuwa anapenda wanaume wakubwa.

Akizungumza na Za Motomoto News, Mwana alisema kuwa, siyo kweli kwamba mwanaume aliyemuoa ni mkubwa kuliko baba yake na hata kama ingekuwa hivyo, haoni shida kwa sababu katika maisha yake anapenda wanaume wenye umri mkubwa maana ndiyo wenye akili, vijana wadogo hawana akili ya maisha zaidi ya fasheni-shoo tu.

“Naona watu maneno yakiwatoka sana kwamba nimeolewa na mwanaume mkubwa kuliko baba yangu, sasa niwaambie tu kuwa haijalishi ila kikubwa ninachojivunia amenipa heshima ya ndoa maana katika wanaume wote niliowahi kuwa nao, huyu ndiye aliyenipenda nami ninampenda na ninamheshimu kuliko chochote.

“Napenda wanaume wakubwa kwa sababu wana akili, lakini wanaume hawa vijana wadogowadogo wao ni fasheni-shoo tu, unakuta anaenda saluni mara tano kwa wiki na mimi mwanamke ninaenda mara tano, sasa hapo kutakuwa na maisha kweli? Ndiyo maana siwapendi,” alisema Mwana.

Mwana alifunga ndoa kwa siri hivi karibuni na mwanaume anayejulikana kwa jina moja la Khamis ambapo picha zake za ndoa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na watu mbalimbali kumshambulia kwamba ameolewa na mzee.