MSIBA WA MASOGANGE: HALI ILIVYO NYUMBANI KWA MZEE GERALD


MWILI wa msanii, Agness Gerald ‘Masogange’ tayari umeshawasili nyumbani katika kijiji cha Utengule, Mablizi, mkoani Mbeya tayari kwa taratibu za mazishi.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao kuzikwa.
Picha zinaonyesha hali ilivyo nyubani kwao marehemu huku ndugu, jamaa, marafiki na wasanii wenzake wakiomboleza msiba huo nyumbani hapo.