Monalisa ameshinda tuzo nchini GHANA

Muigizaji bora na maarufu kutoka Bongo, Yvone Cherry aka Monalisa alieyvutia wengi kwenye uigizaji wake Tanzania ameshinda tuzo Accra nchini Ghana usiku wa kuamkia leo.

Monalisa ameshinda tuzo ya THE APA (The African Prestigious Awards) kwenye kipengele cha Female Movie Star (Msanii Bora wa Kike) na kupitia account yake ya instagram ameshare good news hizo kwa kuandika hiki na kuposti picha akiwa amelala kwenye kitanda hotelini na kujifunika bendera ya Taifa huku akilalia Tuzo.

Kabla ya kwenda nchini Ghana, Mona alikutana na Waziri Mwakyembe na Naibu wake Shonza pamoja na Basata kwa ajili ya kupatiwa bendera ya Taifa na Waziri imesimamia Safari yake ya kwenda kwa kumpatia ticketi na vitu husika katika kwenda kuliwakilisha Taifa.

Hongera Sana Monalisa kwa kushinda tuzo hiyo na unasthili kwani umekua mfano bora katika kiwanda cha Bongo Movie muda woye na kupitia Twitter mwaka jana, Lil Ommy amekutaja kama #NyotaWaMchezo kama Muigizaji Bora wa Kike wa Muda wote, Best Female Actor of all time.

Hongera pia kwa Wazira kwa hatua na jitihada ya kufanikisha Safari ya Monalisa katika kwenda kuliwakilisha na kutangaza Taifa.

Ray pia naye ameshinda katika tuzo hizo kama Male Movie Star.