Man United vs West Brom,Lukaku yuko fiti kwa mechi ya leo

Romelu Lukaku anatarajiwa kuwa fiti 100 baada ya kucheza akiwa anaumwa katika Manchester  Derby wiki iliyopita.
Sergio Romero bado mgonjwa, lakini Phil Jones na   Blind wote wamefanya mazoezi wiki hii na wapo fiti kucheza.
Jonny Evans ana mashaka ya kutocheza leo kutokana na majeruhi ya goti.


Nacer Chadli na Sam Field wamerejea baada ya majeruhi ya muda mrefu - waliitumikia kikosi cha U23 wiki hii - Daniel Sturridge nae yupo fiti kucheza upande wa West Brom.
•West Brom wameifunga Manchester United mara 3 katika mechi 9 zilizopita za ligi tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu - wamefungwa 4 na sare 2. 

 
•Katika mechi 3 walizoshinda West Brom, mbili wameshinda Old Trafford, waliifunga United 2-1 mwezi September 2013, na 1-0 May 2015. 
 
Romelu Lukaku aliifunga United hat trick katika sare ya 5-5, mchezo wa mwisho kabisa wa Sir Alex Ferguson akiwa kocha mnamo mwaka 2013.
 
Mchezo huu utachezwa majira ya saa 12 jioni na utakuwa live kipekee kabisa kupitia