Malkia wa Pop Madonna ameshindwa kuzuia kuuzwa kwa barua ya Tupac Shakur


Malkia wa Pop Madonna ameshindwa kuzuia kuuzwa kwa barua ya Tupac Shakur aliyomwandikia iliyotaja sababu za kuachana naye.

Mwaka jana barua hio aliyoandika Tupac kuhusu mahusiano yake na Madonna pamoja na vitu vingine kama picha, nguo za ndani, vitana na mikanda ya video tofauti za Madonna ilichukuliwa na rafiki yake Darlene Lutz na iliwekwa mnadani na Madonna alitumia pesa, sheria, nguvu na ushawishi wake kuzuia visipigwe mnada. .

Wiki hii jaji Justice Gerald Lebovitz wa Manhattan ametoa majibu ya kesi hio nakusema vitu hivyo vinaweza kuuzwa sababu Madonna alisaini kukubali vichukuliwe na amechelewa kuzuia mnada huo.
Madonna anasema vitu hivyo ni mali zake binafsi za siri na kuuzwa ni kumdhalilisha yeye na familia yake. Barua hio ya Tupac kwa Madonna inaanza kuzwa kwa dola laki moja kwanzia July 2018.