Justin Timberlake kasimulia kitu kilichomkumba mpenzi wake kipindi anajifungua

Justin Timberlake ameweka wazi mssala uliyowakuta yeye na mpenzi wake, Jessica Biel dakika chache baada ya kuingia katika chumba cha kujifungulia hospitalini, mwaka 2015.


Mkali huyo wa RnB aliliambia jarida la Entertainment Tonight kuwa walikuwa wamejiandaa na kuhakikishiwa na madaktari kuwa mke wake angejifungua kwa njia ya kawaida, lakini dakika chache kabla mambo yalibadilika na akatakiwa kufanyiwa upasuaji.

Alieleza kuwa mkewe alifanyiwa upasuaji wa dharura uliofanikisha kumpata mtoto wao wa kiume, Silas.
“Tuliporudi nyumbani tulikuwa tumechoka, tumechanganyikiwa lakini pia tulikuwa na taharuki,” alisema Timberland.