Google wamfanyia party John Legend

Mtandao wa Google kupitia wawakilishi wake nchini Marekani hivi karibuni umeamua kumfanyia sherehe mwanamuziki anayekimbiza kwenye gemu la Muziki wa RnB, John Legend kutokana na wimbo wake uitwao Good Night kupokelewa vyema na mashabiki.

Mbali na sherehe hiyo, mtandao huo pia umesimamia kichupa chake ambacho kilitarajiwa kutoka siku ya ijumaa rasmi kwenye media mbalimbali za burudani duniani na unategemewa kuvunja baadhi ya rekodi za mauzo kwa nyimbo za RnB zilizoachiwa hivi karibuni.

John Legend mwenyewe akizungumzia ujio wake na Mtandao wa Billboard alisema kwamba, anawashukuru mashabiki wake kwa mapokezi mazuri, lakini pia Mtandao wa Google kwa kusimamia kazi yake.

“Ninawashukuru watu wote waliofika kwenye hafla yangu iliyoandaliwa na Google, naombeni mzidi kunipa sapoti kwenye kazi zangu hasa video ambayo tayari inaonesha kila dalili za kuliteka soko la muziki duniani,” alisema John Legend.