Davido apokewa kifalme Zimbabwe kuelekea show yake ya ’30 Billion African Tour’

Davido anazidi kuonyesha kuwa yeye ni mwamba katika muziki wa Afrika. Msanii huyo amepokelewa kifalme nchini Zimbabwe kuelekea ziara yake ya muziki ya The 30 billion African Tour hapo kesho (Ijumaa).
Msanii huyo anatarajiwa kuwasha moto kwenye tamasha lake hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wa Harare International Conference Centre (HICC).

Davido alianza ziara hiyo barani Afrika mwezi Machi 3 ya mwaka huu katika mji wa Kigali nchini Rwanda katika uwanja wa Amahoro ambao ulifurika umati mkubwa wa mashabiki.
Kwa mara ya kwanza ziara ya 30 billion African Tour ilianza kutimua vumbi Juni 23, 2017 katika mji wa Kiev nchini Ukraine na kuhusisha nchi nyingine za bara la Ulaya na Marekani.