Hali ya Mzee majuto yawa mbaya

Dar es Salaam. Muigizaji mkongwe Amri Athumani ‘Mzee Majuto’, amelazwa katika hospitali ya Tumaini Jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa.

Habari hizo zimethibitishwa na mke wake, Aisha Yusufu, alipozunguma na MCL Digital, leo Aprili 23 na alisema mume wake walimpeleka hospitalini hapo saa saba mchana.