Yuko Wapi Darassa Mwenye Muziki Wake?

YUKO WAPI DARASSA MWENYE MUZIKI WAKE

Mwishoni mwa 2016 Tanzania na nchi za Afrika Mashariki ziliipata flava Kali ya Muziki wa Bongoflava kutoka kwa Darassa mara tu alipoiachia Hitsong 'Muziki' ngoma ambayo ilivunja rekodi ya wana-Hip Hop waliofanikiwa kupiga zaidi ya Views nyingi Kwenye mtandao Wa YouTube ndani ya muda Mfupi.

Promo ya Muziki ya Darassa ilikuwa kubwa ukilinganisha na 'Too Much' na 'Kama Utanipenda' aliyomshirikisha @RichMavoko Wa @wcb_wasafi

Muziki ilienda mbali zaidi ya ngoma yeyote Darassa aliwahi kufanya, Muziki ni ngoma ambayo iliongeza umaarufu wa Darassa,

Chati Kadhaa Za Muziki #EastAfrica Ziliongozwa Na #Muziki (Maisha Na Muziki) Ya Darassa.

Kwenye #JiweLaMwezi linaloendeshwa na XXL Ya @cloudsfmtz Mwezi Januari 2017 Muziki ya Darassa ilifanikiwa kutunukiwa cheti cha heshima hiyo.

Licha ya kuwahi kuwa kimya kwa miaka kadhaa kipindi cha nyuma, Ukimya wa muda huu umekuwa ni wa tofauti kabisa,

Hatumsikii Darassa Kwenye Interviews, hatumuoni Kwenye matamasha, hatumuoni wala kumsikia kwenye collabo na wasanii wengine
Mara ya mwisho Darassa kuwa Active Kwenye ukurasa wake wa Instagram(@darassacmg) ilikuwa Agosti, 12, 2017.

Ni Project gani imemfanya Darassa awe kimya kiasi hicho?, U-busy wake umechangia kumuweka mbali na mitandao ya kijamii?, Nina Imani angeweza kuweka msaidizi wa kimitandao ambaye angejaribu kutuficha Project za Darassa lakini atuonyeshe angalau maisha yake ya kawaida.

Ni Kweli ameshindwa kufanya hivyo?

Darassa kama upo mahali umejificha cooking something Iconic Fanya kama unawakumbuka mashabiki wako.

Kama kuna tatizo na Darassa Wenye taarifa sahihi mtupatie majibu.

Namaliza kwa kuuliza tena Safari Hii Kwa Herufi Kubwa. "#YUKOWAPIDARASSA MWENYE MUZIKI WAKE?